Wednesday, July 19, 2017

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: ARSENAL YAIBWAGA BAYERN KWA PENATI 3-2.


Bao la kusawazisha la Dakika ya 94 la Alex Iwobi liliwapa Sare ya 1-1 Arsenal walipocheza na Bayern Munich huko Shanghai na kisha kupata ushindi wa 3-2 kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano kwenye ya kugombea International Champions Cup.

Bayern ndio waliopata Bao la kuongoza kwa Penati ya Dakika ya 9 iliyofungwa
na Robert Lewandowski aliemchambua Kipa Petr Cech.

Penati hiyo ilitolewa kufuatia Ainsley Maitland-Niles kumsukuma Juan Bernat.

Bao hilo lilidumu hadi Dakika 90 kugonga na kwenye Dakika ya 4 ya muda wa Majeruhi Iwobi akaisawazishia Arsenal kwa Kichwa alipounga Krosi ya Aaron Ramsey.

Hadi mwisho Arsenal 1 Bayern 1.

Ndipo ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano na Bayern kukosa 3 zilizopigwa na David Alaba, Sanches and Bernat wakati Ramsey, Nacho Monreal na Iwobi wakiifungia Arsenal.

VIKOSI VILIVYOANZA:

Arsenal XI: Petr Cech; Krystian Bielik, Per Mertesacker, Nacho Monreal, Ainsley Maitland-Niles; Francis Coquelin, Granit Xhaka, Sead Kolasinac, Mesut Ozil; Danny Welbeck, Alexandre Lacazette.
Bayern Munich XI: Tom Starke, Rafinha, Juan Bernat, Mats Hummels, David Alaba; Corentin Tolisso, Franck Ribéry, Javi Martínez, Thomas

Arsenal – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:

13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]

15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]

19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup (1-1, Penati 3-2)

22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)

29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)

30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)

No comments:

Post a Comment