Baraza la wawakilishi la Marekani
limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.
Urusi inaadhibiwa kutokana na kudaiwa
kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa Marekani huku Korea Kaskazini na Iran
wao wakiadhibiwa kufuatia majaribio ya makombora.
Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza
la seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili audhinishe na kuwa sheria
kamili.
Akizungumza katika baraza hilo
wawakilishi David Ciciline kutoka chama
Democratic amesema hatua kamili
zinahitajika kuiwajibisha Urusi.
Amesema hawawezi kuruhusu dola nyingine
kuingilia uchaguzi wao japokuwa Rais wao anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi
uliopita.
Naye Ted Poe kutoka chama cha
Republican amesisitiza kuwa muswada unaihusisha Korea kaskazini pia.
Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya
kimataifa ya bunge la Urusi Duma , Leonid Slutsky amesema hatua hizo mpya
zitazorotesha uhusiano baina ya Urusi na Marekani.
No comments:
Post a Comment