Rais wa Marekani
Donald Trump amesema Venezuela itakabiliwa na hatua za kiuchumi iwapo
itaendelea na mipango yake ya kutaka kuandika upya katiba ya nchi hiyo.
Kufuatia onyo hilo alilolitoa, Rais Trump pia ameupongeza upinzani nchini humo kutokana na kupigania kwake demokrasia na kumuelezea Rais Nicolas Maduro kama kiongozi mbaya ambaye anaota ndoto za kuwa dikteta.
Upinzani
nchini Venezuela umetoa wito wa kufanyika mgomo wa siku moja nchi nzima
siku ya Alhamisi kama sehemu ya kampeni zake kupinga uamuzi huo wa Rais
Maduro kubadili katiba.
Siku ya Jumapili mamilioni ya Wavenezuela
walijitokeza kupiga kura ya maoni isiyo rasmi kupinga pendekezo hilo,
lakini hata hivyo serikali ya nchi hiyo, ikasema zoezi hilo la upigaji
kura si halali.
No comments:
Post a Comment