Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian imekanusha madai kwamba inaisaidia
chama cha upinzani nchini Kenya cha Muungano wa NASA ili kuwekwa kwa
kituo cha kuhesabia kura nchini Tanzania.
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Hassan Abbas amesema kuwa si sahihi kuiunganisha Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu nchini Kenya.
“Suala
hili la kujaribu kuiunganisha nchi inayopenda amani ya Tanzania
kuhusika kwenye Uchaguzi Mkuu wa majirani zetu ni kosa kubwa
lisilofikirika.”
Shutuma
hizi zimeibuka baada ya kuzagaa kwa taarifa kwamba mgombea wa upinzani
Raila Odinga kupitia Muungano wa NASA kuwa wamefanya mpango wa kuweka
kituo cha kuhesabu kura maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam.
Kwa
upande wake, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Alliance, Ekuru
Aukot amesema kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kinyume na Katiba ya
Kenya na Uhuru wa nchi hiyo.
Msemaji
wa Serikali ya Tanzania aliendelea kusema kwamba: “Nina wasiwasi na
taarifa kwamba Muungano wa NASA una mpango wa kuweka kituo cha kuhesabu
kura hapa Tanzania. Suala hili ni sawa na kuidharau Katiba yetu na
kudhalilisha Uhuru wa nchi yetu,” amesema Abbas.
Kuna
taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba hatua hiyo kutoka Muungano wa
upinzani umesababisha mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.
Imesemekana kwamba kwa sababu ya jambo hili, wakubwa serikalini wamekuwa
wakiitaka Serikali ya Tanzania kutoa kauli hadharani kuzungumzia suala
hili.
‘HAKUNA MPANGO WOWOTE ULIOWEKWA KATI YA MAGUFULI NA RAILA’
Katika
mahojiano na kituo cha redio cha Jambo, Raila amesema kwamba chama
tawala cha Jubilee kina wasiwasi wa kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu
kwahiyo wakaamua kuzusha “propaganda” hiyo kuhusu kituo cha kuhesabu
kura nje ya Kenya.
“Sielewi kwa nini watu wanafatilia sana urafiki wangu na Rais wa Tanzania, John Magufuli,” alisema.
“Familia
zetu ni rafiki, na si yeye tu bali hata Rais wa Uganda Yoweri Museveni
ni rafiki yangu wa muda mrefu. Urafiki wangu na yeye unazidi urafiki
kati ya Museveni na (Rais) Uhuru,” alisema.
Raila
ameongeza kuwa yeye ana urafiki na viongozi wengi wa Afrika wakiwemo
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Nana
Akufo-Addo wa Ghana.
“Hamna
mpango wowote kati ya Magufuli mimi. Sisi ni marafiki tu. Chama cha
Jubilee kina njama za kupanga matokeo ya uchaguzi, ndio sababu wanakuja
na mawazo yasiyo na maana kabisa.”
Mgombea
huyo wa Urais kwa tiketi ya Muungano wa NASA amesema kuwa Muungano huo
una mpango wa kuwa na kituo chao ambacho watajumlishia kura zake zote na
kuzilinganisha na zile zitakazokuwa zinahesabiwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi nchini Kenya, IEBC.
“Wana
wasiwasi wa nini? Nini cha ajabu sana kuhusu kuhesabu kura zako mpaka
Serikali nzima iwe na wasiwasi? Eti NASA itaenda kuhesabia kura zake
nchini Tanzania…tatizo liko wapi?” aliuliza.
“Kama
IEBC itatangaza matokeo sahihi, kwanini wanaohaha wawe ni watu wa
Jubilee? Kwanini wawe na wasiwasi wa sisi tunaenda kuhesabu wapi kura
zetu?
“Wao
wanataka yuweke vituo hivyo hapa ili waweze kuvivamia na kuharibu
mashine zetu za kuhesabia. Wajue kwamba tunazo nyingi. Hata kama
watavunja mashine moja au mbili…tutakuwa tumejiandaa,” alisema Raila.
No comments:
Post a Comment