Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amelazimika kukesha ofisini kwake akiwahudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani waliowasilisha matatizo mbalimbali kuhusiana na ardhi.
Waziri
Lukuvi aliingia ofisini majira ya saa mbili asubuhi siku ya Ijumaa
lakini akajikuta akilazimika kufanya kazi hadi saa tisa usiku wa
kuamkia jana Jumamosi.
Wananchi
189 wenye matatizo na kero za ardhi aliitikia wito alioutoa waziri
Lukuvi mwezi Juni, akiwataka watu wote katika mikoa ya Dar es salaam na
Pwani, wenye matatizo ya ardhi, kujiorodhesha ofisini kwake pamoja na
anwani zao na angepanga siku ya kushughulikia matatizo hayo yeye
mwenyewe binafsi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara, sehemu kubwa ya wakazi hao
walilala nje ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam wakisubiri
kuonana na waziri Lukuvi.
Wananachi
wengi wenye matatizo na kero za ardhi waliokesha na Lukuvi walitokea
Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam.
Wananchi
hao wamesifu hatua hiyo ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na
kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea.
Francis
Kamara, mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam, amemuomba Waziri Lukuvi
awawajibishe watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kusababisha
yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment