Matibabu hayo huenda yakashirikisha matumizi ya dawa ama mionzi kulingana na daktari wake.
Uvumbe huo ulipatikana wakati wa upasuaji wa kuondoa damu ilioganda juu ya jicho lake la kushoto.
McCain ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita nchini Vietnam pia alitumikia miaka mitano jela.
Seneta
huyo aliyehudumu kwa mihula sita na kuwa mgombea wa urais wa chama cha
Republican 2008 alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Phoenix katika
jimbo la Arizona siku ya Ijumaa.
Uchunguzi wa tishu ulibaini
kwamba uvimbe wa ubongo unaojulikana kama glioblastoma ulisababisha damu
hiyo kuganda kulingana na taarifa ya kliniki hiyo ya Mayo.
Madaktari wa Seneta huyo wanasema kuwa anaendelea kupona kutoka kwa upasuaji huo na afya yake iko shwari, iliongezea.
Matibabu yake yatashirikisha utumiaji wa dawa na mionzi.
Glioblastoma ni uvimbe mbaya wa ubongo na huongezeka kutokana na umri wa mtu ukiwaathiri wanaume wengi zaidi ya wanawake.
Bwana
McCain ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya sineti kuhusu hudumu za
jeshi alikuwa katika hali nzuri huku akiendelea kupona nyumbani na
familia yake, afisi yake ilisema.
No comments:
Post a Comment