Monday, July 31, 2017

NABII MKUU MH DK. GEORDAVIE: MIMI MAJIRANI ZANGU NI WAISLAMU.

Nabii mkuu Mh. Dk GeorDavie amewataka watu kuwa na upendo kwa majirani zao ikiwa ni pamoja na kusapoti kazi ya Mungu ili iweze kusonga mbele.

Nabii mkuu Mh. Dk GeorDavie ameyasema hayo katika ibada ya jiji iliyofanyika katika hema la kukutania chuo kikuu cha manabii kisongo Arusha ambapo maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali wamehudhuria ibada hiyo ambayo ilikuwa ya unabii mkuu.

Katika ibada hiyo Nabii Mkuu alifundisha na kutamka matamko mbalimbali
ambayo yalikuwa baraka kwa watu wote waliohudhuria ibada hiyo.

Nabii Mkuu Mh Dk. GeorDavie ametangaza kuwa siku ya tarehe 9 mwezi wa 9 mwaka huu anatarajia kufanya kongamano litakalofanyika katika ukumbi wa Mt Meru  ambalo litakuwa kongamano la tisa tangu kuanzishwa kwa makongamano katika huduma ya  Ngurumo Ya Upako.

Pia katika ibada hiyo Nabii mkuu Mh Dk GeorDavie ametangaza kuwa jumapili ya tarehe 13 mwezi wa nane itakuwa siku ya Pipa Day ambapo itafanyika Mjini Mwa Daudi Katika Bonde La Utulivu.

Kwa upande wa watu waliohudhuria ibada hiyo wamesema kuwa wamebarikiwa sana huku wakifurahi kuwepo kwa Nabii Mkuu radioni katika kipindi cha kusapoti Magurudumu ya Radio.

Aidha Nabii Mkuu Mh. Dk GeorDavie ametangaza siku ya leo anatarajia kuwepo radioni katika kipindi cha kusapoti magurudumu ya Radio kuanzia muda wa  saa mbili na nusu usiku ambapo amewataka watu wote kushiriki.

No comments:

Post a Comment