Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amebadilikia Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood na kumtaka
arudishe viwanda mbalimbali ambavyo alibinafsishiwa na serikali kama
ameshindwa kuviendesha.
ambao wataweza kuviendesha.
“Ninarudia
wito wangu niliokwisha kuutoa huko nyuma, kwamba wenye viwanda hapa
Morogoro ambao wameshindwa kuviendesha, na leo nataja akiwemo Mbunge wa
hapa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), narudia akiwemo Mbunge wa hapa wa CCM
ambaye alibinafsishiwa viwanda vingi, kama ameshindwa kuviendesha
avirudishe ili tuwape watu wengine kwa sababu vijana hawa wanakosa
ajira, nazungumza kwa uwazi kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Mbali
na hilo Rais Magufuli amemuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro
SACP - Ulrich Onesphory Matei kuhakikisha askari Mgambo hawawasumbuli
wafanyabiashara wadogo wadogo na amewataka wafanyabiashara hao kutofanya
vurugu wakati utaratibu mzuri unaandaliwa kwa ajili yao.
Rais
Magufuli wakati akiwa katika ziara mkoani Singida aliweka wazi kuwa
yeye anauchukua sana ubinafsishaji na kusema ndiyo umeturudisha nyuma na
kuharibu mipango mizuri ambayo alikuwa nayo Mwalimu Nyerere, huku
akitolea mfano viwanda kadhaa ambavyo vipo Morogoro na vimeshindwa
kuendelezwa na majengo yake kugeuka magodauni ya watu.
No comments:
Post a Comment