Mataifa ya Tanzania na Kenya
yalifanikiwa kuandaa mkutano ambao utapelekea kuondolewa kwa marufuku ya
bidhaa zinazoingia katika mataifa hayo mawili kutoka pande zote mbili.
Waziri
wa maswala ya kigeni na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine
Mahiga alitangaza uamuzi huo jijini Nairobi kufuatia majadiliano kati ya
rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Na
kufuatia hatua hiyo Kenya itaondoa marufuku ya Unga wa ngano na Gesi
inayoingia nchini humo kutoka Tanzania huku Tanzania nayo ikiondoa
marufuku
ya sigara na maziwa kutoka Kenya.
ya sigara na maziwa kutoka Kenya.
Kuongezea, mataifa hayo mawili yataanzisha kamati ya pamoja kuangazia maswala tofauti.
Uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara kati ya Kenya na Tanzania
uliathiriwa kwa muda huku mataifa yote mawili yakiweka marufuku hizo.
Marufuku
ya bidhaa kutoka Tanzania kuingia Kenya ilitokana na wasiwasi wa
kiusalama na ubora wa bidhaa huku Tanzania ikijibu kwa kuweka marufuku
kwa bidhaa za Kenya kama vile matairi ya gari, mafuta ya kupaka mkate na
maziwa.
Tanzania pia imepiga marufuku usafirishaji wa maindi
kutoka Zambia kuelekea Kenya, ambayo inakabiliwa na wakati mgumu wa
ukosefu wa zao hilo muhimu.
Marufuku hizo, ikilingamishwa na idadi kubwa ya bidhaa zinazotoka na kuingia kat
No comments:
Post a Comment