Akitoa
hukumu hiyo Hakimu wa Wilaya ya Serengeti, Amalia Mushi alisema
mshtakiwa ametiwa hatiani katika kesi ya jinai namba 37/2017 kufuatia
ushahidi uliotolewa upande wa Takukuru kutoacha shaka.
Kabla
ya hukumu hiyo, Wakili wa Takukuru, Eric Kiwia alidai kuwa mshtakiwa
aliomba Sh20,000 kutoka kwa Joseph Rhobi mkazi wa kijiji hicho
aliyekamatwa kwa madai kuwa alikuwa akitafutwa na polisi.
Aliendelea
kuwa Rhobi mwaka 2012 alikamatwa na askari wa Kituo kidogo cha Polisi
Machochwe, lakini alitoroka akiwa amefungwa pingu ambazo baadaye
alizisalimisha kwa mtendaji wa kijiji.
Mwanzoni
mwa mwaka huu, Rhobi alihitaji barua ya utambulisho kutoka ofisi ya
kijiji, hivyo mwenyekiti huyo alitoa taarifa polisi na mtuhumiwa
alikamatwa.
Hata
hivyo, Rhobi aliachiwa kwa dhamana hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji
alimdhamini huku akimdai Sh20,000 kumaliza suala hilo hali
iliyosababisha kutoa taarifa Takukuru na kufanikisha kukamatwa.
Mshtakiwa alipelekewa magereza baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh500,000.
No comments:
Post a Comment