Pia
amesema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko la
uhakika hivyo amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda vipate malighafi.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo Jumamosi, Julai 15, 2017 wakati
alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda
cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar Es Salaam.
Alisema
viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani
kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa
zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.
Alisema
kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala
yake wauze katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa
nchini kwa gharama nafuu.
“Pamba
yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa
wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la
uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”
Awali
Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji ya
nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono jitihada za
Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.
Katika
kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani 700,000 kwa mwaka kimeajiri watu 2000 na
kinalipa kodi ya sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu aliwataka
watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe waadilifu.
Pia
Waziti Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha
wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na
viwanda sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.
No comments:
Post a Comment