Thursday, July 27, 2017

WATU WAALIKWA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII HII LEO.

Huduma Ya Ngurumo Ya Upako Duniani siku ya leo kutafanyika ibada ya Chuo Cha Manabii inayoanza kuanzia smuda wa saa sita mchana {12:00} ambapo watu mbalimbali wamealikwa kuhudhuria ibada hiyo.

Akizungumza na N.Y.U Radio Kadinali wa tatu wa Huduma ya ngurumo ya upako Mchungaji Zimani Gervas amesema kuwa ni vyema watu wakahudhuria ibada hiyo kwani watu mbalimbali wameponywa na kuwa huru ikiwa ni pamoja na
kujifunza namna ya kuutunza muujiza.

Aidha Huduma ya nurumo ya upako ibada ya katikati ya wiki ni kila siku za Alhamis na Jumanne ambapo watu kuoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Arusha hufika katika hema la kukutania kwa ajili ya kupokea uponyaji.

No comments:

Post a Comment