Watu wametakiwa kutoogopa kutokana
na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo maishani badala yake wamgeukie
Mungu ambaye anamajibu ya kila mmoja.
Hayo yamesemwa na Mtumishi
mwanafunzi Julieth Mwanyika wakati akihubiri katika ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika
katika hema la kukutania Ngurumo ya upako kisongo Ambapo alifundisha somo
lisemalo”Geuka Maana Yesu ana Majibu yako”.
Akihubiri Mtumishi Julieth amesema
kuwa inawezekana kuwa kuna watu wamepokea habari mbaya ikiwemo Magonjwa,
Madeni, Umasikini, lakini pamoja na hayo hawatakiwi kuogopa kwa kuwa yupo Mungu
anaweza kuwavusha katika mapito hayo.
Naye Mtume Eser Robert akihubiri
ibadani hapo amesema kuwa ili mtu aweze kuzikabili Baraka zake maishani
anahitaji nguvu, Imani, Fedha na Mikopo.
Kwa upande wake kadinali wa tatu wa
huduma ya ngurumo ya upako Mchungaji Zimani Gervas aliwakumbusha watu kutoa
sadaka maalum ya miezi miwili ya kupokea upako wa kukamilisha na kufanikisha
malengo inayotolewa kila siku ya Alhamis kuanzia saa nne Usiku kwa muda wa mwezi
wa sita na wa Saba.
Aidha Chuo cha Manabii ibada ya
katikati ya wiki hufanyika siku za Jumanne na Alhamis ambapo watu kutoka sehemu
mbalimbali huudhuria hemani kwa ajili ya kupokea uponyaji.
No comments:
Post a Comment