Rais wa Ufaransa
Manuel Macron amesema kuwa anaheshimu uamuzi wa rais Trump kujitoa katika
makubaliano ya tabia nchi ya Paris na kwamba Ufaransa itaendelea na juhudi zake
kuhusu makubaliano hayo.
''Kuhusu tabia nchi
tunajua tofauti yetu'', Bwana Macron alisema mjini Paris siku ya Alhamisi ,
akiongezea: Ni muhimu kusonga mbele.
Akizungumza pamoja na
Macron, rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba huenda Marekani ikabadili
msimamo wake lakini hakutoa maelezo ya zaidi.
''Kitu kitafanyika
kwa heshima ya makubaliano ya Paris''.
Bwana Trump
aliongezea: Tutaona kile kitakachofanyika.
Rais huyo wa Marekani
alijiondoa katika makubaliano hayo 2015 mwezi uliopita, akitaka kujadili upya
kwa makubaliano hayo ili kutoiweka Marekani katika hatua isiyo na manufaa kwake
kibiashara.
Bwana Macron alisema
kuwa ni muhimu kuweka makubaliano hayo kando huku viongozi hao wawili
wakizungumza vile watakavyofanya kazi kuhusu maswala kama vile kusitishwa kwa
mapigano nchini Syria na ushirikiano wa kibiashara.
Tuna tofauti zetu;
Bwana Trump ana ahadi za uchaguzi alizowapatia raia wa tafa lake na pia mimi
nilikuwa na ahadi, je vitu hivi vinapaswa kuturudisha nyuma katika maswala
yote? Hapana, alisema Macron.
Bwana Macron na Trump
baadaye walizungumza kuhusu juhudi za pamoja za mataifa hayo katika kukabiliana
na ugaidi na hususan kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.
"Marekani
inahusishwa pakubwa katika vita vinavyoendelea nchini Iraq'', alisema Macron, ''ningependa
kumshukuru rais kwa kila kitu kinachofanywa na wanajeshi wa Marekani katika
eneo hili''.
''Tumekubaliana
tuendeleze na juhudi zetu za pamoja'' ,aliongezea ''husuasan mipango baada ya
vita''.
Bwana Macron alisema
kuwa Ufaransa itaweka mikakati kadhaa ili kusaidia kuimarisha uthabiti katika
eneo hilo.
No comments:
Post a Comment