Meli zinazowasafirisha wanajeshi wa China zinaelekea nchini Djibouti kuweka kambi ya jeshi ya China ambayo ndiyo ya kwanza ya kigeni.
China inasema kuwa kambi hiyo itatumiwa kwa huduma za kulida amani na za kibinadamu barani Afrika na magharibi mwa Asia.Pia itatumiwa kwa ushikiano wa kijeshi, mazoezi ya kijeshi na huduma za uokoaji.
China imewekezaa katika nchi za kiafrika na pia imeboresha kwa haraka jeshi lake miaka ya hivi karibuni.
Halikutaja idadi ya wanajeshi au meli zilizoplelekwa Djibouti au ni lini kituo hicho kitaanza kutangaza huduma zake. Xinhua linasema kuwa kituoa hicho cha Djibouti kinabuniwa kufuatia mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.
Kituo hicho kinaonekana kama hatua ya China ya kuwa na usemi wa kijeshi eneo hilo.
Trump ashtakiwa kwa kuwazuia wakosoaji katika Twitter
Rais wa Marekani Donald Trump kwa muda wa miaka 30 amekabiliwa na zaidi ya na kesi 4,000
Na
sasa mwanabiashara huyo ambaye sasa ni Rais, ameshtakiwa kwa mara
nyingine, baada ya watu saba kumshtaki kwa kuwazuia kwenye akaunti yake
ya twitter.Bwana Trump ni mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijami ambayo anaituma kuwapongeza washirika na kuwashambulia mahasimu wake.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na taasi ya Knight First Amendment Institute, ambalo ni kundi la kupigania uhuru wa kusema katika chuo cha Columbia.
Watumiaji hao saba walisema kuwa akaunti zao zilifungwa na rais au wasaidizi wake, baada ya wao kukejeli au kukosoa ujumbe alioandika Trump.
Watumiaji wa Twitter hawan uwezo wa kuona au kujibu ujumbe katika akaunti zinazowazuia.
Mashtaka hayo ni kuwa kwa kuwazuia watu hawa, Bwana Trump amewazuia kujiunga na majadiliano ya mtandaoni.
Mzee mwenye watoto 100 anasema ana nia ya kuongeza watoto zaidi
Wakati ulimwengu ulipoadhimisha siku ya idadia ya watu duniani mwanamume mmoja alikuwa na sababu 100 za kusherehekea.
Kofi Asilenu mwenye umri wa miaka 80 ni baba wa watoto 100 na wake 12.Anaishi na familia yake katika kijiji chaAmankrom kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu Acca.
Familia yake ni thuluthi moja ya watu 600 katika kijiji hicho.
Anasema kuwa anataka familia kubwa kwa sababu hakuwa na ndugu.
Sina kaka wala shangazi,ndio sababu niliamua kuwa na watoto wengi ndio wapate kunipa maziko yaliyo mazuri nikifa.
Familia hiyo yake hata hivyoy imemgharimu pakubwa. anasema alikuwa mtu mwenye mali, lakini male hiyo ilipungua kutokana na gharama ya kuitunza familia yake kubwa
Kofi Asilenu anaonekama kuwa mwenye afya nzuri na hata anasema kuwa na watoto zaidi.
No comments:
Post a Comment