Kadinali wa tatu wa huduma ya Ngurumo Ya Upako Mchungaji Zimani Gervas
amewaalika watu kutoka sehemu mbalimbali kuhudhuria ibada ya katikati ya wiki
inayofanyika hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha.
Akizungumza na N.Y.U Radio amesema kuwa katika ibada ya katikati ya wiki
watumishi wa mungu hufundisha neno la mungu kwa kifupi na mara baada ya neno la
mungu hupita katikati ya watu kwa ajili ya kuwafungua watu kulingana na
mahitaji yao.
Ameongeza kuwa ibada ya leo itakuwa ni ya baraka, hivyo watu watapokea
miujiza, maongezeko na hatua mpya katika kila eneo.
Aidha amesema kuwa huduma ya ngurumo ya upako ipo kwa ajili ya watu wote
kwani haichagui dini, kabila hivyo nguvu ya mungu ipo kwa ajili ya kuwahudumia
watu wote.
No comments:
Post a Comment